BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya soka ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’  imeibuka na ushindi mnono wa magoli 3-1 dhidi ya wenyeji India katika mchezo wake wa pili wa michuano maalumu ya kimataifa iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka la  nchi hiyo katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa.

Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Maziku Amani dakika ya 21 huku la pili  wakijifunga baada ya beki wao kushindwa kuokoa krosi ya Nickson Kibabage katika dakika ya 28. Bao la tatu la Serengeti  lilifungwa na Asad Juma  dakika ya 48 wakati lakufutia machozi la wageni  likifungwa na Komal Thatal  dakika ya 38.

Kwa ushindi huo, Serengeti sasa wanasubiri angalau sare au ushindi wa mchezo mmoja kati ya miwili, dhidi ya Korea Kusini na Malaysia kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Katika mchezo wa kwanza, Serengeti ilitoka sare ya goli 1-1 dhidi ya  Marekani huku ikitarajia kushuka tena dimbani keshokutwa na Malaysia.

Post a Comment

 
Top