BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
WAZIRI wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Nape Nnauye ameishukuru Serikali ya India kwa kuialika timu ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys katika mashindano maalum ya vijana yatakayoanza Mei 15 nchini India.

Akizungumza kwenye hafla ya kuiaga timu hiyo iliyofanyika uwanja wa Karume Mwenyekiti wa Baraza la michezo Tanzania BMT, Dioniz  Malinzi kwa niaba ya waziri Nape  aliishukuru Serikali ya India kuwapa mwaliko huo kwavile michuano hiyo itasaidia kuiandaa timu kuelekea mashindano ya Afrika kwa vijana yatakayofanyika hapa nchini mwaka 2019.

Kwa upande wake Balozi wa India nchini, Sandeep Arya alisema mashindano hayo yataimarisha ushirikiano wa Tanzania na India katika medani ya michezo hususani vijana kitu kitakacho saidia maandalizi ya vijana hao kuelekea michuano ya Afrika.

Nae Rais wa TFF Jamali Malinzi alisema maandalizi yamekalika kwa asimilia kubwa na vijana wako vizuri wamekaa pamoja kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kumalizika michuano ya Copa Coca Cola mwaka jana hivyo ushiriki wao utakuwa wa manufaa makubwa kwa nchi.

Pia mlezi wa timu hiyo kocha Kim Poulsen alisema wanapata ushirikiano mkubwa toka kwa TFF kitu ambacho ni kizuri na matunda yake yataonekana muda si mrefu.

Serengeti wanaondoka nchini keshokutwa Jumatano tayari kwa michuano hiyo inayoshirikisha mataifa matano huku Tanzania ikiwa ndiyo nchi pekee kutoka barani Afrika na watacheza kwa wiki mbili katika mfumo wa ligi.

Post a Comment

 
Top