BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Nitike Ahazi, Dar
KIUNGO wa zamani wa Simba, Abdallah Seseme ambaye kwa sasa anaitumikia Toto Africans ya jijini  Mwanza, amesema kitu pekee ambacho kinamfurahisha ndani ya kikosi hicho ni ushirikiano pamoja na wachezaji kucheza kwa kujituma.

Akifafanua kauli hiyo, Seseme alisema alipokuwa Simba, alikumbana na ubaguzi na siyo ushindani wa viwango kama mchezaji hivyo ilikuwa ngumu kucheza hata kama kiwango kipo juu.


"Huku mchezaji anaangaliwa kwenye mazoezi akifanikiwa kuonyesha uwezo ndipo anapata nafasi ya kucheza, lakini Simba kama hakuna kiongozi anayekukubali basi inakula kwako," alisema.


Seseme alisema kwa sasa wanapambana kuhakikisha timu inabaki kwenye ligi msimu ujao kwani wameikuta kwenye mwenendo usioridhisha.


"Kuna kazi ngumu kucheza kwenye timu inayofanya kazi ya kujilinda na kushuka daraja, maendeleo yanakuwa tofauti na wale ambao wanawania nafasi za juu pamoja na ubingwa," alisema.


Seseme anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na tayari kuna taarifa za kuwaniwa na Mbeya City ingawa yeye amegoma kukiri hilo.

Post a Comment

 
Top