BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KIUNGO wa Toto Africans ya jijini Mwanza, Abdallah Seseme ana mapango wa kuifikisha klabu hiyo kwenye vyombo vya sheria kwani haijammalizia pesa yake ya usajili.

Toto ilimsajili Seseme akitokea Simba baada ya kumaliza mkataba wake. Usajili wa Seseme ni wa makubaliano ya mwaka mmoja kwa Sh 4 milioni ambapo walimpa nusu ya fedha hiyo.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa Seseme alilipwa Sh 2 milioni huku nyingine wakikubaliana kumalizana kabla ya msimu huu kuanza na sasa unamalizika.

"Ukiachana na pesa ya usajili lakini pia anadai mshahara wa miezi miwili na huu utakuwa wa tatu, walipewa barua kwamba wawe wamekamilisha ndani ya siku saba lakini hawajafanya lolote hivyo suala hili litapelekwa Sputanza muda wowote," alisema mtu wake wa karibu na mchezaji huyo

Alipotakiwa kuthibitisha juu ya hilo Seseme alisema"Ni kweli sijamaliziwa pesa ya usajili pamoja na mishahara yangu sijalipwa. Nasubiri ligi iishe nijue cha kufanya ila taratibu za jinsi ya kudai haki zangu zimeanza kufuatwa, nitaenda sehemu sahihi ya kupata haki zote stahiki," 

Seseme anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu ambapo timu yake imebakiza mechi moja tu dhidi ya Stand United itakayochezwa Mei 21 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Post a Comment

 
Top