BOIPLUS SPORTS BLOG

BASEL, Uswisi
TIMU ya Sevilla ya nchini Hispania imenyakua ubingwa wa Europa ligi kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuichapa Liverpool magoli 3-1 katika uwanja wa St. Jacob Park jijini Basel, Uswis.

Liverpool ambao waliunza mchezo kwa kasi kipindi cha kwanza ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 35 kupitia kwa Daniel Sturridge baada ya kupokea pasi kutoka kwa Phillipe Coutinho.

Kipindi cha pili kilipoanza mshambuliaji Kelvin Gameiro aliisawazishia Sevilla baada ya kupokea pasi toka kwa Mariano huku magoli mengine yakifungwa na Coke dakika ya 64 na 70.

Pamoja na kupata magoli hayo, pia mabingwa hao wa kihistoria walionekana kucheza vizuri kwa muda mwingi kipindi cha pili na kuwafanya majogoo wa Anfield kushindwa kuwazuia wanapofika langoni kwao.

Sevilla imenyakua taji hilo mara nne ndani ya miaka 10 tangu 2006. Imechukua ubingwa huo mwaka 2006, 2014, 2015 na 2016.

Video za mabao yote zinapatikana kwenye ukurasa wetu wa Facebook kwa jina la BOIPLUS BLOGSPOT  au Instagram @boiplus_blogspot

Post a Comment

 
Top