BOIPLUS SPORTS BLOG

MOSCOW, Urusi
ALIYEKUWA mchezaji nambari moja wa tenisi kwa upande wa wanawake Maria Sharapova huenda asicheze tena mchezo huo baada ya kubainika  anatumia dawa za kusisimua misuli.

Raia huyo wa Urusi mwenye umri wa miaka 29 alipatikana na dawa ya Meldonium katika michano ya Australia Open mnamo mwezi Januari.

Alipoulizwa Sharapova iwapo atashiriki katika michuano mingine alijibu hana uhakika kutokana na shutuma zinazomkabili ambazo zinaweza zikaathiri kiwango chake katika michuano mbali mbali ya tenisi.

Machi 12 shirikisho la kimataifa la mchezo wa tenisi ITF lilimpiga marufuku kwa muda Sharapova  kutokana na kashfa hizo za matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku michezoni.

Aidha Sharapova anasubiri kusikia hukumu yake kamili ambayo huenda ikawa adhabu ya kufungiwa  miaka minne japokuwa wataalam wanasema huenda akapewa marufuku ya miezi sita au 12.

Post a Comment

 
Top