BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Akram Msangi, 
KOCHA wa JKT Ruvu, Abdallah 'King'  Kibadeni anaichukulia mechi yake ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Simba ni kama mechi ya fainali kwani anahitaji pointi tatu ili timu yake isishuke daraja.

Simba nao wanahitaji pointi tatu ili washike nafasi ya pili kwani sasa wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 62 nyuma ya Azam wenye pointi 63 wakati tayari Yanga alichukuwa kombe lake.

Kibadeni alisema kuwa wachezaji wake wanafahamu umuhimu wa mchezo huo na  wameahidi kucheza kwa kujitoa ili kuhakikidha wanapata ushindi utakaowasaidia kusalia katika ligi hiyo msimu ujao.

"Ushindi pekee ndiyo utatuhakikishia kubaki katika ligi bila kuangalia matokeo ya wenzetu, tunapambana sana ili kufanikisha hilo," alisema Kibadeni.

Kibadeni aliichukua timu hiyo ikiwa katika hali ngumu mwanzoni mwa mzunguko wa pili wa ligi nakujitahidi kuifikisha hadi nafasi ya 12 baada ya kukusanya pointi 29.

Endapo Ruvu itapoteza mchezo huo  Kagera Sugar na Mgambo wakashinda mechi zao basi maafande hao watashuka daraja.

Post a Comment

 
Top