BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda, Morogoro
BINGWA wa Ligi Kuu Bara, Yanga tayari jana alikabidhiwa kombe lake kwani hakuna timu itakayoweza kufikia pointi zake lakini Simba na Azam leo walikuwa na mechi zao na wote wameshinda.

Simba imeifunga Mtibwa Sugar katika Uwanja wake wa nyumbani wa Jamhuri kwa bao 1-0 bao ambalo lililofungwa kwa kichwa na Abdul Banda dakika ya 70 akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Mohamed Hussein 'Tshabalala'.

Azam ambayo ilikuwa ugenini Uwanja wa Mkwakwani imeifunga African Sports bao 2-1, mabao ya Azam yamefungwa na Erasto Nyoni pamoja na Allan Wanga.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 62  wakati Azam wao wana pointi  63 huku zote zikiwa zimebakiza mechi moja mkononi.


Katika mchezo wa Uwanja wa Jamhuri Simba na Mtibwa zote zilicheza kwa kushambuliana kwa zamu huku zote zikikosa magoli ya wazi kutokana na safu zao za ushambuliaji kutokuwa makini.

Makocha wote walifanya mabadiliko ambapo Mecky Mexime aliwatoa Said Bahanuzi na Hussein Javu nafasi zao ziluchukuliwa na Mzarimu Selemba pamoja na Ally Yusuph.

Jackson Mayanja naye alifanya manadiliko kwa Peter Mwalyanzi nafasi yake ilichukuliwa na Said Issah.

Uwanja wa Sokoine, Prisons imeshinda bao 1-0 dhidi ya Toto Africans ya jijini Mwanza bao la Maafande hao lilifungwa na Jeremiah Juma.

Uwanja wa CCM Kambarage, Kagera Sugar imeshinda bao 2-1 dhidi ga Stand United, mabao yote mawili ya Kagera yalifungwa na Salum Kanoni wakati bao la Stand lilifungwa na Amri Kiemba.

Post a Comment

 
Top