BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
SHUJAA wa Yanga katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi Sagrada Esparanca ya Angola golikipa Deogratius Munishi 'Dida' alisema anajisikia furaha kuisaidia timu yake kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Dida ambaye aliyeonyesha kiwango bora katika mchezo huo pamoja na kupangua penati dakika ya 89, alipokelewa kwa shangwe na mashabiki wa timu hiyo kiasi kwamba ilibidi awekewe ulinzi maalum ili kulinda usalama wake.

Dida alisema "Ukiwa mchezaji na kuisaidia timu yako kufanya vizuri inakupa moyo na kuendelea kujituma zaidi," alisema Dida.

Akizungumzia uwezo wake wa kucheza penati Dida alisema kitu kikubwa nikujiamini unapokuwa langoni na kufanya mazoezi kwa nguvu huku ukithamini kazi yako.

" Nilijiamiani sana langoni nikamsoma mpigaji mwisho wa siku nikafanikiwa kucheza penati ile,"  alisema Dida.

Hii ni mara ya pili kwa golikipa huyo kuibuka shujaa wa timu hiyo kwani hata katika mechi dhidi ya Etoile du Sahel alifanya kazi kubwa.

Post a Comment

 
Top