BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
KIKOSI cha timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars, chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa na Hemed Morocco kinatarajiwa kuondoka kesho saa 12 alfajiri kwenda Nairobi, Kenya kucheza na Harambee Stars katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Mchezo huo ni maandalizi ya kujiandaa kucheza na Misri Juni 4, katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017) wakati Kenya pia itakuwa na mchezo dhidi ya Congo.

Kikosi cha Stars kitakachosafiri ni pamoja na  makipa, Deogratius Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam FC) na Benno Kakolanya (Tanzania Prisons) wakati mabeki ni Mwinyi Haji na Juma Abdul (Yanga), Aggrey Moris, David Mwantika na Erasto Nyoni (Azam FC), Mohammed Hussein (Simba) na Vicent Andrew (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Himid Mao, Farid Mussa (Azam), Jonas Mkude na Mwinyi Kazimoto (Simba), Mohammed Ibrahim na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Ismail Issa (JKT Ruvu), Juma Mahadhi (Coastal Union) na Hassan Kabunda (Mwadui FC).

Washambuliaji ni Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), Mbwana Samatta (KRC Genk), Elias Maguli (Stand United), Ibrahim Ajib (Simba), John Bocco (Azam), Deus Kaseke (Yanga) na Jeremiah Juma (Tanzania Prisons).

Post a Comment

 
Top