BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, Nairobi
TAIFA Stars leo imetoka sare ya bao 1-1 na Harambee Stars katika mechi yao ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa Uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi, Kenya.

Mechi hiyo ni maandalizi ya timu hizo kuelekea mechi ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika ambapo Stars itacheza na Misri Juni 4 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku Harambee ikijiandaa kupambana na Congo Brazaville.

Stars ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao Elias Maguli aliyefunga dakika ya 34 akimalizia krosi ya Juma Abdul wakati Harambee ilisawazisha dakika ya 39 kupitia penalti iliyopigwa na Victor Wanyama.

Penalti hiyo ilipatikana baada ya Abdul kumwangusha Ayub Timbe kwenye eneo la hatari.

Kabla ya Harambee kuivaa Congo siku ya Jumapili, itacheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Sudan Jumanne hapa hapa jijini Nairobi.

Post a Comment

 
Top