BOIPLUS SPORTS BLOG

 Uwanja wa Kaitaba ulioko Bukoba mkoani Kagera umefanyiwa marekebisho makubwa na kuwekewa nyasi bandia.

 Kwa mantiki hiyo msimu ujao wa ligi kuu, timu ya Kagera Sugar haitotangatanga tena kwenye viwanja tofauti, badala yake itatulia katika uwanja wake wa nyumbani.

Timu nyingi za mikoani zinakabiliwa na changamoto ya ubovu wa viwanja. Kama ukarabati wa aina hii ukiendelea kwenye viwanja vingine vibovu kama kile cha Majimaji mjini Songea na vingine, basi kiwango cha soka kinaweza kupanda.

Post a Comment

 
Top