BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu
 Kinda wa Azam Farid Mussa Malick yupo nchini Hispania alikoenda kufanya majaribio katika klabu za Deportivo Tenerife, Las Palmas na Atletic Bilbao

 Farid akiwa na mtoto wa Bakhressa, Yusuf Bakhressa ambaye ameenda Hispania kumshuhudia kijana huyo katika majaribio yakeKwa kuanzia Farid yupo Tenerife ambako taarifa zinasema ameongezewa wiki moja ya majaribio baada ya kuwashawishi wahispaniola hao  Kuna uwezekano mkubwa wa Tenerif kumnunua Farid ingawa atalazimika kuendelea kufanya majaribio katika klabu za Palmas na Bilbao kabla ya kufanya maamuzi Umri mdogo, kasi na nguvu ni baadhi ya vitu vinavyoweza kumfanya Farid apate timu nchini humo Farid anaukosa mchezo wa leo wa timu yake dhidi ya Simba utakaopigwa kwenye dimba la Taifa. Kwa mujibu wa ratiba ya majaribio yake, Farid anaweza kurejea na kuuwahi mchezo wa Fainali ya kombe la FA dhidi ya Yanga

Picha zote kwa hisani ya Azam Fc

Post a Comment

 
Top