BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
MECHI dhidi ya Ndanda Fc na Mabingwa wa Ligi Kuu Bara iliyochezwa jana Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imeingiza Sh 77 milioni, mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya bao 2-2.

Awali mechi hiyo ilipangwa kuchezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara lakini walikubaliana pande zote mbili ichezwe Dar es Salaam ili kuwapa urahisi Yanga kusafiri kwenda Angola kwa ajili ya mechi ya marudiao ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Sagrada Esperanca.

Katika mechi hiyo Ndanda ndiyo walikuwa wenyeji ambapo walipata mgawo wa Sh 25 milioni wakati Yanga wenyewe wamepewa Sh 18 milioni huku habari za ndani zilieleza kuwa Ndanda walikubali kuja kucheza hapa kwasababu waliahidiwa kupewa mapato yote ya mlango.

Ndanda wenyewe kabla ya mechi hiyo walitoa ufafanuzi kwamba kitu pekee kikubwa ukiachana na uzalendo kwa Yanga kwenye michuano ya kimataifa waliangalia fedha watakayopata kwani Yanga ina mashabiki engi ambao wangejitokeza kuishangilia timu yao na kulipa viingilio vikubwa.

''Pesa waliyopata Ndanda si haba ingawa hatuna uhakika na makubaliano yao kama walikubaliana kuachiwa yote ama kupewa yale yao kama wenyeji wa mchezo ambapo mwenyeji anapata pesa nyingi kuliko mgeni,'' alisema kiongozi huyo

Baada ya mechi hiyo Ndanda wataelekea Mbeya kucheza mechi yao ya mwisho dhidi ya Mbeya City. Timu zote mbili hazishuki daraja Ndanda wana pointi 34 City kabla ya mechi yao ya leo jioni dhidi ya Mwadui wamekusanya pointi 33.

Post a Comment

 
Top