BOIPLUS SPORTS BLOG

TASNIA ya michezo imekuwa ikizalisha matajiri wengi sana hapa duniani, soka imekuwa ni ajira kubwa ambayo inaingiza pesa nyingi. Mauzo ya jezi, viingilio vya milangoni, mauzo ya wachezaji, zawadi za ubingwa na vingine vingi vimekuwa vyanzo pesa nyingi.

Mtandao wa Forbes umetangaza orodha mbalimbali kwa mwaka 2014/15 kama ifuatavyo;

WACHEZAJI WANAOLIPWA PESA NYINGI ZAIDI
Straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anaongoza katika orodha ya wachezaji 10 wanaolipwa pesa nyingi zaidi duniani ikijumuisha mishahara na posho zingine. Hii hapa orodha ya wacjezaji hao.

1. Cristiano Ronaldo       $82.1 mil
2. Lionel Messi              $76.5 mil
3. Zlatan Ibrahimovic     $37.1 mil
4. Neymar                      $36.3 mil
5. Gareth Bale              $34.4 mil
6. Wayne Rooney      $25.8 mil
7. Sergio Aguero         $24.4 mil
8. Luis Suarez              $22.8 mil
9. Eden Hazard              $22.2 mil
10. Cesc Fabregas      $20.8 mil

MAUZO YA TIMU
Timu nyingi za soka zimepata mafanikio baada ya kuuzwa kwa matajiri. Chelsea ilinunuliwa na Roman Abramovich mwaka 2003 kwa kiasi cha dola 233 milion  ambapo kwa sasa imefikia thamani ya dola 1.66 bilioni

Familia ya Glazer iliinunua Manchester United kwa dola 1.47 bilioni mwaka 2005. Kwasasa thamani ya mashetani hao wekundu imefikia dola 3.32 bilioni huku Manchester City ambayo ina thamani ya dola 1.92 bilioni ilinunuliwa na Sheikh Mansour mwaka 2008 kwa dola 360 bilioni tu.

Majogoo ya Jiji la London, Liverpool nayo iliuzwa kwa John Henry mwaka 2010 kwa kiasi cha dola 476 milioni lakini ndani ya miaka sita tu thamani yake imefikia dola 1.55 bilioni ambapo mwaka 2011 washika bunduki Arsenal nao waliwekwa sokoni huku tajiri Stan Kroenke akifika dau la dola 1.2 bilioni na kuipandisha thamani hadi dola 2.02 bilioni ya sasa.

AS Roma ilinunuliwa na kampuni ya 'Four-person investor group' mwaka 2011 kwa dola milioni 400. Thamani ya klabu hiyo imepanda na kufikia dola 508 milioni.
Mwaka 2011, Paris Saint-Germain iliuzwa kwa Qatar Sports Investments dola 143 milioni ambayo sasa imepanda thamani hadi dola 814 milioni ikiizidi 
Inter Milan ya tajiri Erik Thohir ambaye mwaka 2013 alimwaga dola 480 milioni, kwasasa Milan ina thamani ya dola 559 milioni.

GHARAMA ZA TIKETI ZA MSIMU MSIMU WA 2015/16
Mashabiki wengi barani Ulaya wamekuwa wakinunua tiketi za msimu mzima kabla hata ligi haijaanza tofauti na hapa nchini ambapo ni ngumu kufanya hivyo kutokana na mabadiliko ya ratiba ya mara kwa mara.

Hii hapa ni orodha ya gharama za tiketi za msimu mzima kwa 10 za juu.
1. AC Milan: $5,177
2. Palmero: $4,305
3. Lazio: $4,304
4. Fiorentina: $3,814
 5. Arsenal: $2,895
6. Tottenham Hotspur: $2,725
7. Inter Milan: $2,588
8. Real Madrid: $2,099
9. Chelsea: $1,798
10. AS Roma: $1,740

TIMU ZINAZOPATA PESA NYINGI KWA MAUZO YA JEZI
Ukiondoa Mbeya City na Simba Sc, hakuna timu nyingine hapa Tanzania iliyouza jezi zake halisi kwa utaratibu unaoeleweka. Barani Ulaya jezi zimekuwa ni chanzo kikubwa cha mapato ya klabu nyingi.

Ifuatayo ni orodha ya timu hizo na pesa wanazopata kwa msimu;

1. Real Madrid $220 mil
2. Manchester United $209 mil
3. Bayern Munich $111 mil
4. Chelsea $99 mil
5. Arsenal $86 mil
6. Barcelona $81 mil
7. Liverpool $79 mil
8. Manchester City $74 mil
9. Juventus $53mil
10. Paris Saint-Germain $51 mil

MAPATO KUTOKANA NA HAKI ZA TELEVISHENI 2014/15
Azam Tv inamaliza mwaka huu mkataba wao na TFF wa kuonyesha mechi za ligi kuu ya Vodacom. Katika mkataba huo kila timu hupewa kiasi cha dola  110 milioni kwa msimu.

Barani Ulaya mambo yalikuwa mazuri msimu wa 2014/15 ambapo timu zilijizolea mamilioni mengi kutokana haki za televisheni. Hii hapa ni orodha ya timu 20 zilizovuta 'mkwanja' mrefu zaidi.

1. Barcelona $192 mil
2. Real Madrid $189 mil
3. Chelsea $167 mil
4. Manchester City $166 mil
5. Manchester United $163 mil
6. Arsenal $163 mil
7. Liverpool $156 mil
8. Tottenham Hotspur $150 mil
9. Southampton $139 mil
10. Everton $136 mil
11. Swansea City $136 mil
12. Newcastle United $131 mil
13. Stoke City $131 mil
14. Crystal Palace $103 mil
15. West Ham United $129 mil
16. Wst Bromwich Albion $123 mil
17. Leicester City $121 mil
18. Aston Villa $116 mil
19. Juventus $113 mil
20. Hull City $112 mil

ORODHA YA TIMU TAJIRI DUNIANI
Real Madrid inaongoza katika orodha ya timu za soka tajiri hapa duniani lakini inazidiwa na timu ya mpira wa miguu wa kimarekani 'American Football', Dallas Cowboys. Ifuatayo ni orodha ya timu tajiri na thamani yake.
1. Dallas Cowboys $4 bil
2. Real Madrid $3.65 bil
3. Barcelona $3.55 bil
4. Manchester United $3.32 bil
5. New England Patriots $3.2 bil

Imeandikwa na Karim Boimanda kwa msaada wa mtandao wa Forbes

Post a Comment

 
Top