BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
KAMATI ya rufaa ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kwa kushirikiana na bodi ya ligi imekaa kwa masaa 72 kupitia rufaa ya kupokonywa alama tatu kwa timu ya Azam baada ya kumchezesha beki Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi tatu za njano.

Ofisa Habari wa shirikisho hilo Alfred Lucas alisema kamati imepitia taarifa za waamuzi na makamisaa na kugundua beki huyo alikiuka kanuni ya 37(4) na 14(37)  ya kucheza michezo mitatu na kuoneshwa kadi ya njano  hivyo adhabu ya kupokwa pointi iko pale pale.

Lucas alizitaja mechi ambazo Nyoni alionywa kwa kuoneshwa kadi ya njano kuwa ni dhidi ya Yanga Agosti 22 mchezo wa ngao ya jamii, Septemba 12 dhidi ya Prison na Machi 16 dhidi ya Costal Union, siku nne baadae akapangwa katika mechi na Mbeya City na kukiuka kanuni za TFF.

Pamoja na kupokwa alama hizo bado wana lamba lamba hao wako nafasi ya pili wakiwa na alama 63 huku wakisalia na mchezo mmoja na endapo watashinda watamaliza ligi na pointi 66.

Azam watashuka dimbani Jumapili ijayo katika mchezo wao wa kufungia msimu dhidi Mgambo JKT ambao wapo kwenye mstari wa kushuka daraja.

Post a Comment

 
Top