BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Nitike Ahazi, Dar
Ally Yusuph 'Tigana' kushoto akiwa na Idd Azan kwenye viwanja vya Leaders

YANGA jana ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kwa kuifunga Sagrada Esperanca ya Angola bao 1-0 lakini kiungo wao wa zamani, Ally Yusuph 'Tigana' amewataka mabingwa hao wa ligi nchini kujipanga upya.

Yanga imetinga hatua hiyo kwa jumla ya mabao 2-1 ambapo mechi ya awali iliyochezaa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam walishinda bao 2-0.

Tigana alisema kuwa kufuzu hatua hiyo ni jambo jema kwa Yanga ila wanapaswa kufanya maandalizi ya maana kwani hatua hiyo upinzani unakuwa mmubwa zaidi.

Tigana aliiambia BOIPLUS: " Yanga inatakiwa kujipanga zaidi kwani kila hatua ina ugumu wake, naamini wana nafasi ya kufanikiwa kutokana na kikosi walichonacho," 

Akizungimzia upande wa Ligi Kuu Bara, Tigana alisema kuwa anasikitishwa na mwenendo wa mbovu wa timu ya Simba na kupoteza mwelekeo kwa kipindi cha miaka minne sasa 

"Ushindani wa kweli na unaoweza kuingiza pesa nyingi kwenye mechi basi ni pale wanapokutana Simba na Yanga, lakini kati ya timu hizo moja ikiwa inafanya vibaya siyo ishara nzuri kwa maendeleo," alisema Tigana

Aliushauri uongozi wa Simba, kutuliza akili na kufanya usajili makini ili mwakani warejee kwenye ushindani.

Post a Comment

 
Top