BOIPLUS SPORTS BLOG

LUBUMBASHI, DR Congo
TIMU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imepata ushindi kiduchu wa goli 1-0 dhidi ya Stade Gabesien ya Tunisia kwenye mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika uliochezwa katika uwanja wa Stade TP Mazembe.

Licha ya kucheza vizuri kwa muda wote wa mchezo wenyeji walipata goli dakika ya 90 baada ya mpira wa kona uliopigwa na Deo Kanda kutua kichwani kwa Juane Bolingi na kuwapatia Mazembe ushindi huo.

Mshambuliaji mtanzania Thomas Ulimwengu alianza katika mchezo huo kabla ya kutolewa kipindi cha pili katika dakika ya 46 na nafasi yake kuchukuliwa na Asante.

Pamoja na ushindi huo bado Mazembe wana kazi ngumu ya kufanya katika mchezo wa marudio utakaofanyika wiki ijayo mjini Tunis  kutokana na waarabu hao kucheza kwa umakini kitu kitakachowapa faida wakiwa kwao.

Mazembe wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya Congo wakiwa na alama 11 baada ya kucheza michezo mitano huku As Vita wakiwa ndiyo vinara wa ligi hiyo.

Gabesien wao  wanashika nafasi ya tisa katika ligi ya Tunisia wakiwa na alama 27 baada ya kushuka dimbani mara 24.

Post a Comment

 
Top