BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasia Congo imefuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika licha ya kukubali kichapo cha magoli 2-1 ugenini dhidi ya Stade Gabesien ya Tunisia.

Wenyeji walionekana kubadilika na kuhitaji matokeo kwa kushambulia mfululizo na kufanikiwa kupata goli la kuongoza dakika ya 28 lililofungwa Youssef Fouzhi kwa mkwaju wa penati baada ya golikipa wa Mazembe kumwangusha mshambuliaji Essif Hicham katika eneo la hatari.

Kipindi cha pili timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu huku wenyeji wakiwa bora zaidi, dakika ya 53 nusura mtanzania Thomas Ulimwengu aipatie goli Mazembe lakini mpira aliopiga kufuatia kona iliyochongwa na Rainford Kalaba, ulipaa juu ya lango.

Dakika ya 61 Gabesien walipata goli la pili kupitia kwa Adjei baada ya mabeki wa Mazembe kuchelewa kuondoa hatari langoni mwao.

Jonathan Bolingi aliifungia Mazembe goli lililoivusha timu hiyo katika dakika ya 70 kwa shuti kali la mita sita lililomshinda mlinda mlango wa Gabesien.

Mazembe walishinda goli 1-0 katika  mchezo wa awali na hivyo kuwavusha katika hatua inayofuata kwa faida ya goli la ugenini.

Post a Comment

 
Top