BOIPLUS SPORTS BLOG

✏Nitike Ahazi, Dar
UBINGWA ambao Yanga wametwaa wa Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho la soka (TFF) umewapaisha nyota wa timu hiyo ambao wametamka wazi kuwa umewaweka kwenye ulimwengu mwingine wa soka la kimataifa na watajivunia watakaporudi kwao.

Kiungo wa timu hiyo Mzimbwabwe Thaban Kamusoko, ameiambia BOIPLUS kuwa wamepata heshima kubwaa kwa ubingwa huo ambao pia umechangiwa na umoja wao.

"Jambo la kwanza namshukuru Mungu aliyetuwezesha, lakini najisikia vizuri kwamba hata nikirejea nyumbani ama wakipata habari za Yanga, tutaheshimika nchini kwetu, kwani wataona kweli tupo Tanzania kwa ajili ya kazi," alisema.

Kamusoko alisema kuwa ubingwa huo umewajenga kisaikolojia kujiamini kufanya vema hatua ya makundi kwenye michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo karata yao ya kwanza itachezwa Juni 17 nchini Algeria.

"Nadhani hata TP Mazembe, itachukulia Yanga ni timu yenye heshima yake kulingana na kile tulichokifanya, morali hii itatusaidia kujituma na kupambana ili furaha ya mashabiki iendelee.

"Nawashukuru mashabiki wa Tanzania wana upendo ambao ulisababisha  nijitume ili huduma yangu iwafurahishe kwani wanapenda sana mpira wa miguu na ndiyo maana walikuwa wanajitokeza kwa wingi," alisema Kamusoko.

Post a Comment

 
Top