BOIPLUS SPORTS BLOG

KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imetangaza kesho Mei 27,  kuanza kwa mchakato wa kuchukua fomu za kugombea uongozi katika Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam inayotarajia kufanya uchaguzi mkuu Juni 25.

Nafasi zinazogombewa ni pamoja na nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe nane  wa Kamati ya Utendaji.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Aloyce Komba fomu zinapatikana katika ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, Vilevile utaratibu unafanyika ili fomu ziweze kupatikana katika tovuti ya shirikisho
www.tff.or.tz

Fomu zinapatikana kwa gharama ya Sh 200,000 kwa nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti, Sh 100,000 kwa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 31 Mei.

Post a Comment

 
Top