BOIPLUS SPORTS BLOG

✏Mwandishi Wetu
WAAMUZI kutoka nchini Gabon ndiyo watakaochezesha  mchezo wa kimataifa kufuzu mataifa ya Afrika  kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Misri utakaofanyika Jumamosi Juni 4,  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo utaanza saa 10.00 jioni  ambako mwamuzi wa kati atakuwa ni Meye Bastrel atakayesaidiwa na Mihundou Ganther na Vinga Theophile wakati mwamuzi wa akiba  atakuwa Otogo Eric.

Wakati waamuzi wote wanatoka nchini Gabon, Kamishna wa mchezo huo ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.

Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuipokea timu ya taifa ya Misri inayotarajiwa kuingia kesho Juni 1 ambapo wataweka kambi  katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, Dar es Salaam.

Taifa Stars imeweka kambi Hotel Urban Rose ambayo pia iko katikati ya jiji la Dar es Salaam tangu iliporejea kutoka Kenya jana  ambako ilicheza  na Harambee Stars na kutoka sare ya goli 1-1.

Post a Comment

 
Top