BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
ALIANZA Juuko Murshid ambaye aliitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda ambacho kilikuwa na mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Zimbabwe.

Baadaye alifuata kipa wao Vincent Angban raia wa Ivory Coast pamoja na winga Brian Majwega aliyedaiwa kuondoka kwa kutumia usafiri wa barabara wakati Angban yeye akipanda Mwewe (Ndege).

Jumamosi ya wiki iliyopita mshambuliaji wao Raphael Kiongera aliondoka usiku kurudi kwao baada ya kuona hapewi taarifa yoyote na viongozi wake ingawa ligi inapomalizika wachezaji wa timu zote huenda kwenye mapumziko kuungana na familia zao.

Jana Jumatatu kiungo wao raia wa Zimbabwe, Justice Majabvi aliondoka kurudi kwao hivyo watakaobaki jijini Dar es Salaam wakisubiri kukatiwa tiketi na klabu ni Mrundi Emiry Nimubona na Hamis Kiiza.Habari za uhakika ambazo BOIPLUS imezipata ni kwamba wachezaji hao wote wameondoka kwa kujitegemea kwa maana ya kujikatia tiketi wenyewe baada ya kuona hawaambiwi chochote klabuni hapo.

"Hakuna mchezaji aliyeambiwa kuwa wanatakiwa lini warudi kambini kwani mshahara ukitoka nadhani kila mtu atapewa taarifa, ligi imeisha na kila mchezaji anapaswa kwenda kuona familia yake hivyo walioondoka wameamua wao kuwahi tu," alisema kiongozi huyo.

Kiongera yeye amethibitisha kurudi kwao hivyo hivyo Majwega na Juuko pamoja na Angban wakati Nimubona yeye alisema bado yupo jijini Dar es Salaam anaendelea kuwasikilizia viongozi wake ambao hawajamwambia jambo lolote hadi sasa ikiwemo kupewa tiketi kwa ajili ya safari yake kurudi Burundi.

Hata hivyo wachezaji ambao wanadaiwa kubaki kwenye kikosi cha Simba msimu ujao ni wawili pekee kati ya hao saba ambao ni Angban na Majabvi huku wengine huenda wakaachwa ingawa haijatangazwa rasmi.

Post a Comment

 
Top