BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF), limemteua Michael  Wambura kuwa Kamishna wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Rwanda na Msumbiji unaotarajiwa kufanyika jijini Kigali, Juni 3.

 Wambura ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), atakuwa Balozi mzuri katika mchezo huo unaokutanisha timu za nchi ambazo Tanzania imepakana nazo.

Msumbiji iko Kusini mwa Tanzania wakati Rwanda iko Magharibi mwa Tanzania.

Post a Comment

 
Top