BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
BARAZA la wazee wa klabu ya Yanga limekipongeza kikosi cha timu hiyo kwa kufika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika pamoja na kuchukua ubingwa wa ligi huku ikisalia na michezo mitatu.

Katibu wa Baraza hilo  mzee Ibrahim Akilimali alisema wameona ni busara kuwapongeza wachezaji wao kwa kazi kubwa waliofanya ya kuwapa furaha baada ya kunyakua ubingwa wa ligi mara mbili mfululizo.

" Wanajeshi wetu walipambana sana mpaka kufikia hapa na pia uongozi ulikuwa madhubuti kuhakikisha timu inafanya vizuri kwa kuwapa wachezaji mazingira mazuri ya kufanya kazi "alisema Akilimali.

Katika hatua nyingine Katibu huyo aliwataka wanachama wa klabu hiyo kutokubali kugawiwa kuelekea katika uchaguzi mkuu mwezi ujao baada ya kuonekana makundi miongoni mwao.

" Kuelekea uchaguzi mkuu wa klabu kuna makundi yanatokea lakini nawaomba wanachama wenzangu tusikubali kugawanywa tuiweke Yanga yetu mbele" alisema Mzee Akilimali.

Aidha Mzee Akilimali alisema kuna baadhi ya vyombo vya Habari vinaleta choko choko ili kuwaharibia timu kuelekea uchaguzi wao.

Post a Comment

 
Top