BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Nitike Ahazi, Dar
YANGA tayari ni mabingwa na keshokutwa Jumamosi watacheza na Ndanda Fc lakini Nahodha wao Nadir Haroub 'Canavaro' ametamka kuwa hawatachafua rekodi yao kwa kufungwa na Ndanda.

Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo siku hiyo Yanga watakabidhiwa rasmi kombe lao kabla ya Jumapili kuelekea Angola kwenye mechi yao ya marudiano ya kimataifa dhidi ya Esperanca.

Akizungumza na BOIPLUS, Canavaro alisema "Tumedhihirisha kwamba hatubahatishi, tunaendelea na majukumu ya kimataifa, lakini 
nazihimiza timu nyingine zilizokosa ubingwa msimu huu zijipange kwa ajili ya msimu ujao ili soka liwe na ushindani,"


Cannavaro alisema mechi ambayo ilikuwa muhimu kwao ni ile ya Mbeya City ambayo walishinda bao 2-0 na kujihakikishia ubingwa lakini pia aliishauri timu hiyo kuongeza nguvu kwa lengo la kuibua ushindani kwenye ligi kama ilivyokuwa moto kipindi ambacho ilipanda daraja na kushiriki Ligi Kuu Bara.

"City, wajipange kinachotakiwa kwenye mechi ya VPL ni ushindani utakaofanya ligi iwe bora naamini msimu ujao utakuwa wa tofauti kwani timu zitaenda kusajili na kujipanga upya.


kikubwa nawaomba Watanzania wajitokeze kwa wiki Jumamosi kutupa sapoti kwani hatutaki kuchafua rekodi, tutaendeleza ushindi,'' alisema Canavaro nawaomba Watanzania wajitokeze kwa wiki Jumamosi kutupa sapoti kwani hatutaki kuchafua rekodi, tutaendeleza ushindi,'' alisema Canavaro.

Post a Comment

 
Top