BOIPLUS SPORTS BLOG

✏Bakari Kagoma, Dar
TIMU ya Yanga imetawazwa kuwa mabingwa wapya wa Kombe la FA baada ya kuifunga Azam Fc magoli 3-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ambao ulianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu, Yanga ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya tisa kupitia kwa Amisi Tambwe baada ya kupokea mpira wa krosi kutoka kwa beki Juma Abdul.

Baada ya goli hilo Yanga waliendelea kulisakama lango la Azam pamoja na kumiliki mpira huku mabeki wa kati wa Azam wakionekana kushindwa kuhimili kashkashi za akina Donald Ngoma.

Kipindi cha pili dakika ya 47 Tambwe aliwaamsha tena Yanga baada ya kufunga goli la pili kufutia krosi ya Haruna Niyonzima na dakika moja baadae Didier Kavumbagu aliipatia Azam bao pekee kufuatia kazi nzuri ya Ramadhani Singano.

Deus Kaseke alifunga goli la tatu dakika ya 80 baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa Simon Msuva na kumuacha golikipa Aishi Manula akiwa hana la kufanya.

Hilo linakuwa taji la pili kwa Yanga msimu huu baada ya wiki iliyopita kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom.

Bingwa mtetezi wa kombe hilo ilikuwa ni timu ya JKT Ruvu iliyonyakuwa mara ya mwisho mwaka 2002 kabla ya kusimama na kuanza tena msimu huu.

Post a Comment

 
Top