BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
KATIKA kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa FA, Yanga imeamua kukigawa kikosi chake mara mbili nyota wa timu hiyo wakibaki jijini Dar es Salaam wakati wenzao wakienda Songea kumalizia mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Majimaji itakayochezwa kesho Jumapili.

Nyota hao wamebaki kwa ajili ya mechi yao ya fainali ya Kombe la FA itakayochezwa Jumatano kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya Azam FC.

Waliobaki ni Kevin Yondani, Thaban Kamusoko, Donald Ngoma, Vincent Bossou, Simon Msuva, Juma Abdul, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Benedictor Tinnoco na Malimi Busungu ambaye ni mgonjwa.

Meneja wa Yanga, Saleh Hafidh alisema ''Kuna baadhi ya wachezaji wamebaki Dar es Salaam kwa ajili ya mechi ya Jumatano huku tumekuja na baadhi tu ila hao ndiyo waliobaki wengine wote tumekuja nao,''

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara walitua jana wakitokea Angola ambako walikuwa na mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisbo barani Afrika ambapo wameitoa Sagrada Esparanca na kutinga hatua ya robo fainali.

Post a Comment

 
Top