BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
MECHI kati ya Yanga na Ndanda iliyotakiwa ichezwe Jumamosi kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara sasa itachezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Taarifa za ndani kutoka Shirikisho la Soka nchini (TFF) zinasema kuwa mabadiliko hayo ni kutokana na makubaliano ya timu zote mbili ambazo zimeafikiana kwamba mechi hiyo ichezwe Taifa.

Sababu kubwa zipo mbili ni kwamba kuwapa nafasi Yanga ya kujiandaa na mechi yao ya marudiano ya kimataifa dhidi ya Esperanca ya Angola na pili ni kukabidhiwa kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu Bara ambapo tayari Yanga ndio mabingwa.

Baada ya makubaliano hayo Ndanda wao wataondoka Mtwara kesho Jumatano ili kusogea maeneo ya jirani na jiji la Dar es Salaam ambapo itapiga kambi yake mkoani Pwani.

Katika kanuni ya ligi hakuna madhara ya mabadiliko ya Uwanja utakaochezwa mechi ilimradi timu husika zitafikia makubaliano na uwanja uliopendekezwa unakubalika na vigezo kwa ajili ya kucheza mechi.

BOIPLUS iliwasiliana na uongozi wa Ndanda ambao ulikiri juu ya kuridhia mabadiliko hayo ya Uwanja.

Post a Comment

 
Top