BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu, Dundo
PAMOJA na kufungwa bao 1-0 ugenini na Sagrada Esperanca ya Angola lakini Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga wamefuzu hatua ya makundi itakayochezwa mwezi ujao.

Mechi hiyo imemalizika muda si mrefu nchini Angola ambapo Yanga wamepata faida ya kusonga mbele baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mechi yao ya awali iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Bao la Waangola hao lilifungwa na Love Kabungula dakika ya 25 na walichoamua Yanga ni kucheza kwa kulinda zaidi goli lao baada ya kushindwa kusawazisha bao hilo.

Dakika ya 89, Esperanca walipata penati iliyopigwa na Kabungula lakini kwa umahiri na umakini mkubwa, kipa wa Yanga Deogratius Munishi 'Dida' aliweza kuipangua.

Timu nyingine zilizofuzu hatua hiyo ni Mounana ambayo imeifunga Etoile du Sahel bao 1-0 pamoja na Madema SC iliyoifunga Mamelodi Sundowns bao 1-0.

Post a Comment

 
Top