BOIPLUS SPORTS BLOG

Nitike Ahazi, Dar
KIRAKA wa Yanga, Pato Ngonyani, amesema kitendo cha timu yake kutwaa ubingwa mara mbili mfululizo kimemuongezea CV ya ubora wa kazi yake.

Akizungumza na BOIPLUS, Pato alisema kuwa timu inapotwaa ubingwa wa ligi inaongeza sifa ya mchezaji hasa kwenye rekodi zake kitaifa na kimataifa.

"Kwa wenzetu nje rekodi za ubingwa ni muhimu haijalishi kulikuwa na ushindani wa kiasi gani kwenye nafasi yangu, ila katika CV, lazima nitaandika kwamba nimewahi kutwaa ubingwa mara kadhaa nikiwa na Yanga," alisema.

Pato alisema kuwa Yanga inazidi kumng'arisha kimataifa zaidi kutokana na timu hiyo kushiriki michuano ya kimataifa ambapo alidai kwamba hata akikosekana kikosi cha Taifa Stars bado anafaidika na timu yake.

"Yanga inatosha kunitangaza ingawa napambana siku moja nije nitumikie timu ya Taifa, ila kwa sasa Yanga  inanifanya kazi yangu ijulikane umbali mrefu," alisema.

Alisisitiza kwamba anaamini nyota yake iking'ara anaweza kuonekana na klabu za nje na ndoto yake ya kucheza nje ikatimia.

Post a Comment

 
Top