BOIPLUS SPORTS BLOG

✏Bakari Kagoma, Dar
WACHEZAJI wapya waliosajiliwa na timu ya Yanga Hassani Kessy na Juma Mahadhi wametambulishwa mbele ya wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kabla ya kuanza mechi ya fainali ya kombe la FA dhidi ya Azam katika uwanja wa Taifa.

Wachezaji hao walipewa jezi za timu hiyo zenye rangi ya kijani na kushangiliwa na mashabiki wa timu hiyo katika jukwaa la VIP A.

Afisa habari wa timu hiyo Jerry Muro ndiye aliyewatambulisha kwa wapenzi na  wanachama hao huku akiwapiga vijembe watani wao wajadi Simba.

Wapenzi na wanachama waliokuwa jukwaa la VIP A waliwatuza pesa wachezaji hao huku wakionesha nyuso za furaha na matumaini kwa wanandinga hao ambao wataanza kuitumikia timu hiyo msimu ujao.

Kwa upande wao wachezaji hao walionekana kufurahi baada ya kushangiliwa na mashabiki pamoja na kupewa pesa.

Post a Comment

 
Top