BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar

MFUNGAJI bora wa michuano ya kombe la FA, Atupele Green amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia maafande wa JKT Ruvu ya mkoani Pwani.

Atupele ambaye alikuwa na msimu mzuri na klabu yake ya Ndanda FC msimu uliopita alifanikiwa kuibuka mfungaji bora wa kombe la FA baada ya kufunga magoli matano.

Mshambuliaji huyo ameithibitishia BOIPLUS kuwa tayari amesaini mkataba wa mwaka mmoja huku akishindwa kuweka wazi dau lake la usajili na maafande hao, kwa sasa anakuwa mchezaji mpya wa timu hiyo ambaye atavaa magwanda msimu ujao.

"Ni kweli nimesaini mwaka mmoja na JKT Ruvu, tulifikia makubaliano vizuri nikasaini mkataba, msimu ujao nitawatumikia," alisema Atupele.

Atupele alikuwa mhimili mkubwa wa klabu ya Ndanda katika safu ya ushambuliaji lakini baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita 'Wanakuchele' hawakukaa nae ili  kuongeza kandarasi mpya.

Post a Comment

 
Top