BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar

MSHAMBULIAJI wa Ndanda FC ya mkoani Mtwara Atupele Green amekanusha uvumi ulioenea kuwa yuko mbioni kujiunga na Majimaji 'Wanalizombe' toka Songea.

Kwa takribani wiki moja kumekuwa na taarifa za mfungaji bora huyo wa michuano ya kombe la FA kujiunga na Miamba hiyo ya mkoani  Ruvuma yenye historia kubwa katika ligi kuu Tanzania bara.

Atupele ameiambia BOIPLUS kuwa hajafanya makubaliano yoyote na Majimaji wala viongozi wao hawajamtafuta kuzungumzia suala la kuhitaji saini yake.

"Sijui chochote kuhusu hilo, sijawasiliana na mtu yoyote toka huko ndiyo kwanza nasikia kwako kuwa wananihitaji," alisema Atupele.

BOIPLUS ilifanya jitihada za kuwatafuta viongozi wa 'Wanalizombe' kuzungumzia suala hilo lakini hakuna aliyepatikana kwenye simu.

Aidha mshambuliaji huyo alisema kuwa endapo viongozi hao watamfuata na kukubaliana maslahi yake yupo radhi kuwatumikia.

Atupele ni miongoni mwa washambuliaji wazawa waliofanya vyema msimu uliopita kiasi cha timu nyingi zinazoshiriki ligi kuu kuanza kumtolea macho.

Post a Comment

 
Top