BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
KIPA Mpya wa Yanga, Beno Kakolanya ametaja sifa ambazo anapaswa kuwa nazo mrithi wake baada ya yeye kusaini mkataba wa miaka miwili na Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga.

Beno ametaja sifa hizo kuwa ni nidhamu pamoja na kujituma vinginevyo kipa huyo hataweza kumudu mikikimikiki ya ligi ambayo ina upinzani mkubwa. Prisons imebakiwa na makipa wawili Aron Kalambo ambaye ni kipa namba mbili na Mohamed Yusuph.

Beno ameiambia BOIPLUS kuwa makipa wawili waliopo Prisons kwasasa wana uwezo mkubwa wa kucheza ila tu wazingatie hayo mambo mawili kwani yatawasaidia kwa maisha yao ya soka.

''Mtu yoyote tu pale anaweza kudaka na anaweza kurithi mikoba yangu na anaweza kucheza kutoruhusa magoli mengi, kikubwa kinachotakiwa ni kujituma, nidhamu pamoja na  ushirikiano kwa wachezaji, viongozi mpaka mwalimu ndo muhimu zaidi,'' alisema Beno.

Akizungumzia maisha ya Prisons ambayo ndiyo timu yake ya kwanza kumpeleka kucheza VPL alisema: ''Nimejifunza vitu vingi sana ndani ya Prisons, kwanza nimeishi nao kwa upendo pia ni timu ambayo inamfanya mchezaji awe mvumilivu kutokana na ubora wao,''

Beno anaamini ubora wa makipa wa Yanga Ally Mustafa 'Barthez' na Deo Munishi 'Dida' ndiyo utamfanya apambane ili apate namba.

Post a Comment

 
Top