BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
YANGA wamenasa saini ya kipa wa Prisons ya Mbeya na Taifa Stars, Benno Kakolanya asubuhi ya leo na kumpa mkataba wa miaka miwili.

BOIPLUS ilimtafuta Kakolanya ambaye alikiri kukamilisha 'dili' huku akiweka wazi ada ya kusaini kuwa ni Sh 35 milioni na mshahara Sh 1 milioni kwa mwezi.

"Kweli nimemalizana nao na saizi nipo kwenye gari narejea Mbeya. Nitakuwepo kule kwa siku mbili tu kwani Alhamisi natakiwa kuripoti klabuni," alisema Kakolanya

Kakolanya alionyesha uwezo mkubwa msimu huu akicheza mechi 19 za ligi kuu na kufungwa mabao manane tu huku akiisaidia Prisons kumaliza katika nafasi ya nne mbele ya Mtibwa iliyomaliza ikiwa nafasi ya tano.

Yanga sasa itakuwa na makipa wanne ambao ni Ally Mustapha 'Barthez', Deogratius Munishi 'Dida', Benedicto Tinoco anayedaiwa kuwa atatolewa kwa mkopo katika moja ya timu na Kakolanya

Post a Comment

 
Top