BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
NAHODHA na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria, Stephen Okechukwu Keshi amefariki dunia asubuhi ya leo akiwa na umri wa miaka 54.

Emmanuel Ado, kaka wa marehemu aliliambia gazeti la PREMIUM TIMES kuwa Keshi amefariki ghafla kwa ugonjwa wa shinikizo la damu.

Keshi alimpoteza mke wake Mrs Kate Keshi Disemba 9, 2015 kwa ugonjwa wa kansa na leo familia hiyo inaomboleza kifo cha kiongozi wao.

Post a Comment

 
Top