BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
MATAJIRI wa jiji, Machester City wameamua kuanza kuijenga timu yao lakini kwa staili ya kuzibomoa timu nyingine huku wakianza na wajerumani Borussia Dortmund inayosuasua kurejesha makali yake.

City imeingia klabuni hapo na kumnyakua kiungo wao mahiri, Ilkay Gundogan ambaye amepewa mkataba wa miaka minne kwa ada ya uhamisho ya paundi 21 milioni.

Usajiki wa kiungo huyu wa Ujerumani mwenye miaka 25 unakuwa wa kwanza kwa kocha Pep Guardiola tangu alipojiunga na City.

Gundogan atakosa michuano ya Euro pamoja na mechi za kwanza za msimu ujao wa ligi kufuatia kuumia goti mazoezini mwanzoni mwa mwezi Mei.

Post a Comment

 
Top