BOIPLUS SPORTS BLOG

TURIN, Italia

CHELSEA imeshindwa katika mbio za kumnyakua  Miralem Pjanic toka AS Roma baada ya kiungo huyo kujiandaa kujiunga na  Juventus muda wowote kuanzia sasa. 

Kocha mpya wa 'The Blues' Antonio Conte ambaye atakiongoza kikosi hicho msimu ajao amekuwa akimkubali sana kiungo huyo na alitaka kuungana nae Stamford Bridge.

Raia huyo wa Bosnia amefunga magoli  10 na kusaidia upatikanaji wa mengine 12 katika   Serie A msimu uliopita.

Mkurugenzi wa michezo wa Juve Beppe Marotta alisema "Tumekamilisha kila kitu kuhusu mchezaji huyo kwa ada ya Pauni milioni 30 na muda  mfupi ujao atafanyiwa vipimo vya afya". 

" Timu nyingi zilikuwa zikimuhitaji kama vile PSG, Chelsea na Barcelona lakini sisi tulikuwa haraka zaidi na kufanikiwa kumpata" alisema Marotta.

Wiki iliyopita Wakala wa mchezaji huyo Adis Junozovic alisema kupitia tovuti ya Bosnia N1 kuwa wamefikia makubaliano na Juve na kila kitu kilikuwa kinaenda sawa kwa mteja wake huku akitanabaisha kuna asilimia kubwa ya kiungo huyo kujiunga na 'Vibibi vizee vya Turini' msimu ujao.

Post a Comment

 
Top