BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa FC Platinum ya Zimbabwe Aubrey Chirwa yupo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha usajili wa kujiunga na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga huku ikifahamika kuwa ameshamalizana na wababe hao wa Jangwani.

Usajili wa nyota huyo umefanyika kwa haraka zaidi ili kuweza kupeleka jina lake shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF ili kuweza kumtumia katika michezo yake ya kimataifa ya kombe la shirikisho.

Chirwa ambaye alitengeneza kombinesheni nzuri na Donald Ngoma walipokuwa katika kikosi cha FC Platinum atakuwa msaada mkubwa kwa mabingwa hao hasa kwavile tayari anafahamiana nao vizuri.

Chirwa ameingia kandarasi ya miaka miwili na nusu na kujikusanyia kitita cha dola 100,000 hivyo kuwa miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa pesa nyingi na mabingwa hao.

Chirwa anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Yanga toka FC Platinum baada ya Donald Ngoma na Thaban Kamusoko.

Post a Comment

 
Top