BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar

KIUNGO mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga Obrey Chirwa ataondoka usiku wa leo kuelekea nchini Uturuki kujiunga na wenzie walioweka kambi kwa ajili maandalizi ya mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe.

Yanga imepoteza mchezo wa kwanza katika michuano hiyo baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 ugenini dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria na sasa inajiwinda na mechi ya pili dhidi ya mabingwa hao wa kihistoria wa Klabu bingwa Afrika utakaofanyika Juni 28 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Chirwa aliyejiunga na Yanga akitokea FC Platinum ya Zimbabwe alikuwa akisubiri vibali vitakavyo muwezesha  kuwatumikia mabingwa hao wa ligi kuu na kombe la FA msimu uliopita.

Ofisa Habari wa klabu hiyo Jerry Muro alisema kuwa tayari wameshakamilisha kila kitu kuhusu vibali vya mchezaji huyo na sasa yuko huru kuwatumikia vijana hao wa Jangwani.

"Mchezaji wetu anaondoka leo saa 5 usiku kuelekea nchini Uturuki kujiunga na wenzake baada ya kupata vibali vya kuitumikia Yanga, na sasa yuko yuko tayari kuitumikia timu yetu," alisema Jerry.

Chirwa anatarajiwa kuongeza ubunifu katika safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo imekuwa ikipoteza nafasi nyingi za kufunga, safu hiyo kwasasa ipo chini ya Donald Ngoma, Amis Tambwe na mawinga Simon Msuva na Deus Kaseke.

Chirwa ni mchezaji wa tatu toka FC Platinum kujiunga na mabingwa hao baada ya Thaban Kamusoko na Donald Ngoma.

Post a Comment

 
Top