BOIPLUS SPORTS BLOG

TOULOUSE, Ufaransa
ITALIA imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Euro 2016 baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Sweden katika uwanja wa Stade de Toulouse.

Mshambuliaji mwenye asili ya Brazil Eder ndiye aliyefunga goli la ushindi dakika ya 88 baada ya kupokea pasi safi toka kwa Simon Zaza na kupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango.

Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic ameshindwa kuisaidia Sweden kupata ushindi baada ya kufanya majaribio kadhaa langoni mwa Azzuri lakini ulinzi uliokuwa chini Georgio Chellin ulikuwa imara zaidi.

Italia inaongoza kundi E ikiwa na alama sita ikifuatiwa na Ireland ya kaskazini yenye alama moja sawa Sweden huku Ubelgiji ikiburuza mkia kwa kutovuna alama yoyote.

Kesho Ireland ya kaskazini itamenyana na Ubelgiji katika mchezo wa kundi E ili kila timu kuwa sawa katika idadi ya michezo.

Post a Comment

 
Top