BOIPLUS SPORTS BLOG

LIVERPOOL, Uingereza
KLABU ya Everton imethibitisha kumteua kocha Ronald Koeman kuwa meneja wao kwa mkataba wa miaka mitatu. 

Koeman anachukua nafasi ya  Roberto Martinez ambaye alifutwa kazi mwezi uliopita  Goodison Park baada ya mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Kwa mujibu wa Sky sports Everton watawalipa Southampton pauni milioni tano kwa kuvunja mkataba na beki huyo wa zamani wa Uholanzi.

Martinez ambaye amebakisha miaka mitatu katika mkataba wake aliifikisha Everton nusu fainali ya kombe la FA na Capital One huku akimaliza nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Mholanzi huyo amekuwa na miaka miwili ya mafanikio na Southampton baada ya kufanikiwa kumaliza nafasi ya sita msimu uliopita na kuiwezesha kucheza Europa ligi msimu ujao.

Post a Comment

 
Top