BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza

GWIJI wa Manchester United  Ryan Giggs atamthibitishia kocha mpya  Jose Mourinho uamuzi wa kuachana na klabu hiyo wakikutana uso kwa uso wiki ijayo.

Giggs amekuwa kocha msaidizi  United kwa miaka miwili chini ya kocha  Louis van Gaal, lakini baada ya kutimuliwa kwa Mholanzi huyo na kibarua kupewa Mourinho inaonekana hana nafasi ndani ya mashetani Wekundu. 

Giggs anaamini wakati wake wa kuwa kocha mkuu umefika katika timu nyingine kwakua ameshapata uzoefu katika klabu ya Man United.

Kuondoka kwa Giggs kunampa  nafasi Mourinho ya kumchukua mtu wake anaye muamini sana Rui Faria kuwa msaidizi wake  msimu ujao baada ya kufanya kazi nae kwa muda mrefu.

Endapo  Giggs ataendelea kusalia kwa Mashetani hao itabidi abadilishiwe majukumu kwakuwa hawezi kuwa msaidizi wa Mourinho.

United imemtaarifu winga huyo wa zamani kuwa anapaswa kuchagua nafasi mpya ndani ya klabu huku habari za ndani zikisema atapelekwa katika  'Academy' ya timu hiyo.

Post a Comment

 
Top