BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
 Mshambuliaji wa Coastal Union ya Tang, Abasarim Chidiebele

TIMU ya Stand United nayo imeanza usajili wa kimya kimya ambapo kocha wao Mfaransa Patrick Liewig ametoa mapendekezo ya majina matano ya wachezaji wapya atakaosajiliwa kwenye kikosi chake cha msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Liewig hajafikiria kabisa kuchukuwa wachezaji kutoka timu za Dar es Salaam hasa Simba na Yanga ila ameangalia zaidi timu za mikoani kama Toto Africans, Coastal Union, Kagera Sugar.

Baadhi ya wachezaji aliowapendekeza na wameanza kufanya nao mazungumzo ni Salehe Adeyum, Abasarim  Chidiebele (Coastal Union). Chidiebele amewahi kuichezea timu hiyo kwa mafanikio makubwa, Miraji Musa (Toto Africans) na Adam Kingwande.

Habari kutoka ndani ya timu hiyo zinasema kuwa Liewig ataongeza wachezaji wawili wa kigeni kutoka Ivory Coastal pamoja na wengine kutoka Kanda ya Ziwa ambao waliwachukuwa kutokana na programu maalumu iliyoendeshwa kati ya Acacia na Sunderland.

''Hawa wachezaji tisa waliochaguliwa kwenye programu hii maalumu ya kukuza vipaji watafanyiwa majaribio na watakaofanya vyema tutawasajili na kuungana na timu. Kuna wengine wataongezewa mikataba hivyo kikosi kitakuwa kimetimia,'' alisema kiongozi huyo.

Post a Comment

 
Top