BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda
 Nahodha wa Stars ambaye pia ni straika wa KRC Genk ya Ubelgiji ameamua kuchagua jozi hii ya viatu kwa ajili ya kuwamaliza Mafarao wa Misri. Ni kiatu chepesi kinachotulia mguuni, nyota wengi wametokea kukipenda.


Kinda Juma Mahadhi anaweza kuanzia benchi kutokana na kukosa uzoefu, lakini hilo halimzuii kujiandaa tayari kwa kulisaidia taifa lake pale atakapohitajika, amechagua viatu hivi.


 Kiungo Jonas Mkude yeye anasema akinyanyuliwa tu na kocha Boniface Mkwasa, basi ataiweka humu miguu yake ili 'kukata umeme' na kuhakikisha wamisri hawapati mawasiliano kati ya mabeki na washambuliaji


John Bocco yeye humwambii kitu kwa hii NIKE, tarajia kumuona leo akipeperusha bendera ya Taifa letu


 Kama atapangwa leo utakuwa mara yake ya pili kuichezea Stars, huyu ni Mohamed Hussein 'Tshabalala', mlinzi wa kushoto wa Simba anayegombea namba na Haji Mwinyi katika kikosi cha Mkwasa


 Mkwasa anatarajia kuwavuruga wamisri kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo kwa kuwashambulia, licha ya viungo, kocha huyo anamtegemea Juma Abdul katika kuanzisha mashambulizi hayo, na hili hapa ndilo 'Jembe' atakalotinga staa huyo


 Kiungo wa Mtibwa Shiza Kichuya karata yake imeangukia hapa. Kumbe siri ya zile mbio zake inaanzia kwenye hii NIKE


 'Silent Killer' Jeremia Juma, ukimuachia nafasi atakuonyesha matumizi sahihi ya hii kitu NIKE Mercurial


 Mashambulizi ya Stars leo yataanzia pembeni ambako pia kuna Thomas Ulimwengu 'Bufallo' , lakini kinachompa kiburi Staa huyo wa TP Mazembe ya DRC ni ubora wa viatu hivi ambavyo amepanga kuvitumia leo


 Kipa wa Prisons ambaye ameitwa kwa mara ya kwanza timu ya Taifa, Benno Kakolanya, chaguo lake la leo ni kiatu hiki kilichotengenezwa na kampuni ya NIKE


 Deus Kaseke yeye kapita kwenye njia walizopita Samatta na Ulimwengu.


Himid Mao 'Ninja' yeye bado hajajua atavaa viatu gani kwa ajili kuangusha 'minara ya simu' ya wamisri ili wasiwasiliane kabisa pale katikati ya uwanja. Baada ya kuukagua uwanja ndipo atachagua kati ya hizi jozi mbili hapa

Post a Comment

 
Top