BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, Dar
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limetoa kalenda ya msimu mpya wa mashindano na matukio ambayo yataanza baada ya mapumziko ya wachazeji yanayoishia Juni 10.

Kalenda inaonesha kipindi kinachofuata sasa ni usajili unaotarajiwa kuanza Juni 15. Usajili huo unaanza na uhamisho wa wachezaji kuanzia Juni 15 hadi Julai 30.

Kwa mujibu wa Kalenda hiyo, timu ambazo hazishiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 zitaanza kutangaza wachezaji walioachwa kuanzia Juni 15 hadi Juni 30.

Kwa upande wa timu zitakazoshiriki Ligi Kuu, watatumia kipindi cha Juni 15 hadi Juni 30 kutangaza usitishwaji wa mkataba ya wachezaji. Usajili wa wachezaji wapya utaanza Juni 15 hadi Aigosti 6, kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.

Pingamizi itakuwa ni Agosti 7 hadi 14 kabla ya kuthibitisha usajili kwa hatua ya kwanza kati ya Agosti 15 na Agosti 19 wakati usajili hatua ya pili utaanza Agosti 17 hadi Septemba 7 na utafuatiwa na kipindi cha pingamizi hatua ya pili kuanzia Septemba 8 hadi Septemba 14.

Septemba 15 hadi Septemba 17 itakuwa ni kipindi cha kuthibitisha usajili hatua ya pili.

Ratiba hiyo inasema kwamba timu zinatakiwa kuandaliwa  kuanzi Juni 15 hadi Julai 15 ambako kuanzia Julai 16 hadi Agosti 14 ni kipindi cha mechi za kirafiki za ndani na nje. Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itatoka kati ya Julai 16 hadi Agosti 14.

Post a Comment

 
Top