BOIPLUS SPORTS BLOG

PARIS, Ufaransa
ITALIA imeianza vyema michuano ya Euro baada ya kuichapa Ubelgiji magoli 2-0 katika uwanja wa Stade's de Lumiere's katika mchezo wa kwanza wa kundi E.

Emanuele Giaccherin ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwafungia Italia goli la kwanza dakika ys 32 baada ya kupokea pasi toka kwa Leornado Bonucci upande wa kulia.

Ubelgiji walikuja juu baada ya goli hilo lakini ukuta wa Italia uliokuwa chini ya Giorgio Chielini, Bonucci na Barzagli ulikuwa makini kuondoa hatari toka kwa akina Eden Hazard na wenzie.

Huku watu wakiamini mchezo huo ungeisha kwa ushindi wa goli moja Graziano Pelle aliipatia goli la pili Italia dakika za nyongeza na kuwafanya Azzuri kuibuka na ushindani wa magoli 2-0.

Italia wanaongoza kundi E wakiwa na alama tatu wakifutiwa na Ireland na Sweden waliotoka sare ya goli 1-1

Post a Comment

 
Top