BOIPLUS SPORTS BLOG

PARIS, Ufaransa
MABINGWA watetezi wa michuano ya Euro timu ya Taifa ya Hispania imevuliwa ubingwa baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-0 toka kwa Italia katika uwanja wa Stade de France.

Azzuri wamelipa kisasi baada ya kukubali kipigo cha magoli 4-0 toka kwa Hispania katika mchezo wa fainali mwaka 2012 zilizofanyika nchini Poland na Ukraine.

Vijana wa Antonio Conte walipata goli la kwanza kupitia kwa beki Georgio Chiellini dakika ya 33 kabla ya Graziano Pelle kufunga la pili katika dakika za nyongeza na kuhitimisha ushiriki wa mabingwa hao.

Golikipa David De Gea alifanya kazi ya ziada kuokoa michomo ya Waitaliano ambao walikuwa imara karibuni kila idara.

Italia itaungana na mataifa mengine nane katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo itakayofikia tamati Julai 10 nchini Ufaransa.

Post a Comment

 
Top