BOIPLUS SPORTS BLOG

TURIN, Italia
JUVENTUS inahitaji dau la kuvunja rekodi ya dunia la pauni 160 milioni toka  Real Madrid ili kumuachia kiungo wake  Paul Pogba katika dirisha hili la usajili.

Kocha wa Madrid  Zinedine Zidane na Rais Florentino Perez wamemfanya kiungo huyo kuwa mchezaji wao namba moja msimu huu sambamba na mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya ufaransa Dimitri Payet.

Los Blancos wanatarajia kumuuza  James Rodriguez ili kupata fedha ya kumchukua Pogba, lakini bei hiyo inaweza kutibua dili hilo huku kiungo huyo pia akiwindwa na Manchester United, Manchester City, Chelsea na Paris Saint Germain.

Gazeti la  Marca la nchini Hispania limeripoti kuwa  Madrid haitokuwa tayari kutoa kitita hicho kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 huku wakala wake Mino Raiola akisema dili hilo litakamilika.

Ripoti zinasema kuwa Juve wanajua Real hawana longo longo katika matumizi ya pesa hasa wanapo muhitaji mchezaji kama walivyowauzia Zidane mwaka 2011 kwa kuvunja rekodi ya dunia ya wakati ule lakini katika hili miamba hiyo ya Hispania inaweza ikachemka.

Zidane ni shabiki mkubwa wa kiungo huyo kitu kinachoipa Real nafasi ya kupata saini yake huku wote wakitokea taifa la Ufaransa.

Pogba kwa sasa yupo na kikosi cha Ufaransa kinacho shiriki michuano ya Euro na tayari ameshaisaidia kupata ushindi wa michezo yake yote miwili ya awali.

Post a Comment

 
Top